NA TIMA SALEHE, DAR ES SALAAM

KIKOSI cha Azam fc, kitashuka dimbani kuvaana na Horseed ya kutoka nchini Somalia kesho.

Mchezo huo wa Kombe la Shirikisho hatua ya awali unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex, Septemba 11 saa 1:00 usiku.

Biashara United wao wakitarajia kuvaana na FC Dikhil ya nchini Djibout leo nchini huko saa 12 jioni za Tanzania.

Azam wao watacheza kwenye Dimba lao la nyumbani Azam Complex, jijini Dar es Salaam.

Kocha msaidizi wa Azam FC, Bahati Vivier alisema wamefanya maandalizi yakutosha na wanaendelea kujiandaa kwa mchezo huo.

Alisema wanahitaji matokeo mazuri kwenye mchezo huo wakwanza ili kujiweka kwenye nafasi nzuri.“Hakuna timu ambayo haitaki ushindi malengo yetu ni kushinda, tutacheza viuzri kuhakikisha tunatimiza malengo hayo,” alisema