MUNICH, Ujerumani
KLABU ya Bayern Munich imeungana na Paris Saint-Germain na Real Madrid kuwania saini ya beki wa Chelsea, Atonio Rudiger ambaye mkataba wake unaelekea ukingoni huko Stamford Bridge.

Bayern wanafuatilia hali ya Rudiger ambaye mpaka sasa hajaongeza mkataba na Chelsea na mkataba wake wa sasa unakamilika msimu ujao wa joto.

Miamba hiyo imekuwa ikiwasiliana na wakala wa Rudiger na kaka yake, Sahr Senesie, lakini, mazungumzo hayo ni ya awali kwa sasa.

Upande wa Julian Nagelsmann unamchukulia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kama mbadala mzuri wa Niklas Sule endapo anatarajiwa kuondoka Allianz Arena msimu ujao wa joto.

Kama ilivyo kwa Rudiger, mkataba wa Sule unamalizika mwishoni mwa msimu, na amezuia mazungumzo na bado hajaamua ikiwa anataka kuendelea na mabingwa hao wa Bundesliga.

Mazungumzo yanaendelea kati ya Chelsea na Rudiger kuhusu kuongeza mkataba, ingawa ‘Blues’ wanabakia waangalifu juu ya madai yake.Mchezaji mwenyewe anafurahia kubakia London, lakini, anajua kutokana na umri wake, mkataba wake unaofuata unaweza kuwa wa mwisho wa fedha nyingi. (Goal).