WASHINGTON, MAREKANI

RAIS wa Marekani Joe Biden ametangaza mpango wa kuzitaka kampuni zenye wafanyakazi 100 au zaidi kuhakikisha wafanyakazi wao wanapata chanjo dhidi ya virusi vya korona au kuonyesha matokeo hasi ya kipimo angalau mara moja kwa wiki.

Biden alielezea hatua hiyo mpya ambayo huenda ikahusisha wafanyakazi wapatao milioni 80.

Ofisa mwandamizi wa utawala anasema waajiri wasiotii wanaweza kutozwa faini za hadi dola 14,000 kwa kila ukiukaji.

Marekani hivi karibuni imeshuhudia kuongezeka kwa visa vya virusi vya korona kutokana na aina mpya ya Delta inayoenea kwa kasi.Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa kinasema idadi ya vifo kwa siku ilizidi 1,600.