BRASILIA, BRAZIL

RAIS Jair Bolsonaro wa Brazil amebadilisha kauli juu ya mashambulizi yake kwa taasisi za serikali, akisema kwamba vijembe vyake dhidi ya Mahakama ya juu vilitokana na hamasa ya mkutano.

Katika maelezo yake ya kimaandishi, kiongozi huyo wa siasa kali za mrengo wa kulia alisema hana nia ya kupambana na mamlaka yoyote ya nchi hiyo na anaziheshimu kwa kuwa ndizo msingi wa uendeshaji nchi.

Kwenye hotuba mbele ya wafuasi wake katika maandamano ya Siku ya Uhuru mjini Sao Paulo, Bolsonaro aliwaambia hata kama hawataki kupambana na yoyote, lakini hawatoruhusu mtu yoyote kuutia hatarini uhuru wao, akimaanisha Jaji Alexandre de Moraes, anayesimamia kesi dhidi yake.

Bolsonaro alimtaka mkuu wa mahakama hiyo ya juu kumuwajibisha Jaji Moraes, ama wakabiliane na matokeo mabaya.