NA MADINA ISSA
CHAMA cha Mapinduzi Wilaya ya Amani kichama, kimekemea na kulaani vikali vitendo vya udhalilishaji kwa watoto vinavyoendelea kufanyika katika visiwa vya Zanzibar.
Akizungumza na Mabalozi wa Jimbo la Mpendae, Katibu wa CCM Wilaya ya Amali, Ali Salum Suleima, kikao ambacho kilifanyika katika Ukumbi wa CCM, jimbo la Mpendae, wilaya ya Mjini Unguja.
Alisema, vitendo hivyo vimekuwa vikiongozeka siku hadi siku ambapo hivi karibuni kumejitokeza tukio la kushitusha la mtoto wa mienzi tisa kulawitiwa bila ya huruma.
Alisema, kila kukicha vitendo vya udhalilishaji vimekuwa vikishamiri jambo ambalo linasababisha pia kukosa kwa viongozi waliokuwa imara na wenye uwezo wa kuja kuongoza nchi.
Alisema, licha ya serikali kulikemea suala hilo, bado vimeonekana kuongezeka, jambo ambalo limekuwa likiwavunja moyo viongozi wa juu kwani wamekuwa msatari wa mbele kulikemea suala hilo.
“Rais, wetu Dk. Hussein Mwinyi, amekuwa mstawi wa mbele katika kulikemea, ambapo sasa imeanzishwa mahakama ya udhalilishaji kwa lengo la kuwapa adhabu watuhumiwa hawa, ila matendo yameongezeka, hili linasikitisha kwa kweli” alisema.
Aidha alisema, serikali inakemea lakini baadhi ya wananachi wamekuwa wakitia pamba masikio yao na kuona matendo hayo yamekuwa yakiendelea katika mitaa mbalimbali huku wafanyaji wa vitendo hivyo wamekuwa wakiachiwa.
Hivyo, ni vyema kwa mabalozi kuwa mstari wa mbele katika kulikemea suala hili, ili kuona vitendo hivyo vinamalizika.
“Vitendo hivi vinaongezeka kila uchao licha ya serikali kulipinga kwa kasi, hivyo sio vyema kuliona suala hili linaendelea na isitoshe tuangalieni utu kuliko kitu” alisema.