NA MWANDISHI WETU

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi jana amefanya uteuzi wa nafasi mbalimbali za uongozi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na kusainiwa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena Ahmed Said imeeleza Dk. Mwinyi amemteua Dk. Juma Yakuti Juma kuwa Naibu Katibu wa Baraza la Mapinduzi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Dk. Mwinyi amemteua Suleiman Ali Suleiman kuwa Naibu Katibu Msaidizi wa Baraza la Mapinduzi (Sera, Ufuatiliaji na Tathamini).

Katika uteuzi huo, Dk. Othman Abbas Ali ameteuliwa kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Yussuf Ibrahim Yussuf ameteuliwa kuwa Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Saumu Khatib Haji ameteuliwa kuwa Kamishna Idara ya Bajeti na Haji Ali Haji ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Idara ya Sera za Kodi na Fedha.

Naye Suleiman Mohamed Rashid ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Idara ya Uendeshaji na Utumishi na Mohamed Hassan Khamis ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Idara ya Mipango, Sera na Utafiti.

Siti Abbas Ali ameteuliwa kuwa Kamishna wa Idara Mipango ya Kitaifa, Maendeleo ya Kisekta na Kupunguza Umasikini, Ahmed Makame Haji ameteuliwa kuwa Kamishna wa Idara ya Ukuzaji Uchumi na Khamis Issa Mohammed ameteuliwa kuwa Ofisa Mdhamini Tume ya Mipango, Pemba.

Naye Dk. Mohamed Juma Abdalla ameteuliwa kuwa Katibu Mtendaji Kamisheni ya Utalii, Hafsa Hassan Mbamba ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Idara ya Masoko na Aviwa Issa Makame ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Idara ya Mipango na Maendeleo ya Utalii.