ZASPOTI
BOSI wa zamani wa Misri, Hossam El Badry, amesisitiza uvumi kwamba alikuwa na uhusiano mbaya na mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah ni wa uongo na haukuwa nyuma ya kufutwa kazi hivi karibuni.
El Badry (61), alikuwa analinoa taifa hilo la Kiafrika kwa miaka miwili kabla ya kuondolewa mnamo Septemba 6. Ulikuwa uamuzi ambao ulitoka nje ya hilo. Mafarao walikuwa wamepigania sare 1-1 na Gabon katika mechi ya kufuzu Kombe la Dunia.
Chini ya saa 24 baadaye kocha wao aliwekwa ‘gerezani’ akiwa hajashindwa katika michezo yake 10 aliyoiongoza. Uvumi ulianza kuenea kuwa uhusiano wa beki huyo wa zamani wa Misri na Salah ulikuwa nyuma ya kutimuliwa.
Lakini kocha huyo ambaye ameifundisha miamba ya Misri ya Ahly kwa nyakati tatu tofauti ametoa kauli ya kukana hilo.
“Habari nyengine zilibadilishwa, na kufukuzwa kwangu kulikuwa kwa kushangaza, kwa hivyo watu walitia chumvi,” alisema. “Hakukuwa na matatizo kati yangu na Salah hata kidogo. Nilizungumza naye muda si mrefu uliopita. Ilisemekana kwamba Salah alikuwa akidai wachezaji wengine kuitwa, na hii sio kweli.
“Wanasemaje kwamba uhusiano wangu na Salah ni mbaya, na aliteuliwa kuwa nahodha na mimi?”
Salah amechukua mchezo wake kwa kiwango chengine tangu ajiunge na Liverpool katika msimu wa joto wa 2017. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 amefunga mabao 130 kutoka mechi 209 kwenye mashindano yote.
Amekuwa shujaa kwa nchi yake, akikwamisha mabao 45 ya kimataifa kutoka michezo 71. Nyota huyo wa zamani wa Roma alicheza kwenye mechi ya mwisho ya El Badry akiwa amekosa ile ya awali kwa sababu ya vizuizi vya ‘corona’.
Alikosa michezo mingi chini ya kocha huyo aliyezaliwa jijini Cairo kwa sababu ya jeraha. Lakini, akiunga mkono madai yake ya hapo awali, El Badry aliweka wazi kwanini mshambuliaji huyo wa ‘wekundu’ hao alipaswa kuwa nahodha wake. (Goal).