LONDON, England
BEKI wa zamani wa Manchester United, Rio Ferdinand, amesisitiza kwamba klabu za Manchester United na Liverpool zimsajili, Raheem Sterling ili kuokoa kipaji chake baada ya winga huyo kuachwa gizani na Manchester City.
Sterling aliisadia ManCity kutwaa mataji tangu atue Etihad akitokea Liverpool mwaka 2015, lakini, muda wake wa kucheza umepunguzwa na kocha, Pep Guardiola.
Winga huyo wa kimataifa wa England amecheza mara mbili kwa kuanza katika michezo sita ya ManCity kwenye michuano yote msimu huu.”Yupo Raheem Sterling, amepoteza kujiamini kwa sababu ameondolewa kwenye kikosi”, alisema, Ferdinand kupitia chaneli yake ya FIVE ya Youtube.
“Kama ningekuwa Liverpool, ningemnunua Sterling hata kesho tu… kama ningekuwa yeye nisingekwenda Barcelona au Real Madrid kwa sasa ndiyo maana nasema Liverpool au United watamchukua.Sterling alimaliza kama mfungaji bora wa ManCity kwa misimu miwili katika Ligi Kuu ya England akiwa na magoli 20 katika michezo 33 na alizidiwa na Ilkay Gundogan (13) msimu uliyopita yeye akiwa na mabao 10. (Goal).