LONDON, England

JACK Grealish nyota mpya ndani ya kikosi cha Manchester City ambaye aliibuka huko akitokea klabu ya Aston Villa, ameweka wazi kuwa ana uwezo wa kumpindua beki wa aina yoyote akiwa anakimbia ndani ya boksi.

Hii inatokana na bao lake alilofunga kwa kuwachambua mabeki kadhaa na kuiwezesha Manchester City kushinda mabao 6-3 dhidi ya RB Leipzig kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya Jumatano iliyopita.

Kiungo huyo mwenye miaka 26 alikuwa akicheza mchezo huo ndani ya Uwanja wa Etihad na kueleza kuwa ni furaha kwake kufunga.

“Mpira ulikuja kwangu na ninapokuwa katika nafasi hiyo nikikimbia ninaweza nikampita yeyote tukikabiliana mmoja mmoja, nina furaha kupata bao,” amesema.