MANCHESTER, England
KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola, amesema, hakuridhishwa na Riyad Mahrez, kwa kupuuzia maelekezo yake katika kipindi cha kwanza katika ushindi wa magoli 6-3 dhidi ya RB Leipzig katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya juzi.

Meneja huyo kutoka Hispania anaingia kwenye kumbukumbu za kushinda michezo 87 katika michuano ya Ulaya huku akimtoa Arsene Wenger katika nafasi ya tatu.
Guardiola japo alikuwa anaongoza mpaka dakika ya 63 kwa magoli 4-2, lakini, hakufurahishwa na kiwango cha Mahrez na kumuita kumfokea.

Grealish pia alikumbana na hasira za Guardiola, meneja huyo hakufurahishwa na kasi ya ushambuliaji wake.Ushindi huo haukumfanya Guardiola kutulia na alipoulizwa kwa nini aliwafokea wachezaji hao, tulizungumza jinsi tutakavyocheza, lakini, hawakufanya kama tulivyo kubaliana.

Magoli ya Manchester City yalifungwa na Nathan Ake, Jack Grealish, Joao Cancelo, Gabriel Jesus na Mahrez huku magoli ya Leipzig yakifungwa na Christopher Nkunku, aliyefunga goli zote tatu.Wakati huo huo, meneja wa Chelsea, Thomas Tuchel, amesema, Romelu Lukaku ndiye aina ya mchezaji Chelsea aliyekuwa amekosekana klabuni hapo baada ya mchezo dhidi ya Zenit.

Goli la kichwa la Lukaku katika kipindi cha pili liliwahakikishia Chelsea ushindi wa 1-0 dhidi ya Zenit katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.”Uchezaji wa Romelu haukuwa rahisi. Hatukumtengenezea nafasi nyingi, lakini, yeye ni aina ya mtu asiyepoteza ujasiri na imani. Na ndio sababu yeye ni mshambuliaji wa kiwango cha ulimwengu”, alisema, kocha mkuu huyo wa Chelsea.

“Ni mchezaji wa muhimu, ni rahisi kama hivyo. Haupati washambuliaji wengi wa ubora wake”, aliongeza, Tuchel.Chelsea inashika nafasi ya pili katika kundi ‘H’ nyuma ya Juventus yenye magoli mengi zaidi, akifuatiwa na Zenit kisha Malmo.(Goal).