TOKYO, JAPANI

MAOFISA wa wizara ya afya ya Japani wanasema zaidi ya wagonjwa 2,200 wa virusi vya korona kote nchini humo wako mahututi.

Idadi ya wagonjwa wa virusi hivyo ambao wanahitaji kuwekewa mashine za moyo na mapafu za ECMO ilifikia rikodi ya juu ya wagonjwa 161 Jumamosi.

Shimizu Keiki, daktari anayesimamia shughuli za hospitali za ECMO anasema ikiwa idadi ya wagonjwa mahututi itaendelea kuongezeka,haitowezekana kuchukua hatua zaidi.

Shimizu ameongeza kuwa wafanyakazi wake wanakaribia kuelemewa.

Mamlaka nchini Japani waliripoti visa vipya vya maambukizi 12,908 Jumapili.

Wizara ya afya inasema watu 2,207 nchini kote wapo mahututi kutokana na virusi hivyo.

Hiyo ni pungufu ya wagonjwa 16 kutoka Jumamosi, ilipokuwa idadi kubwa zaidi kuwahi kutokea tangu kuanza kwa janga hilo.