BAADA ya kipindi cha kama miaka miwili mitatu ya ahuweni ya kudhibitiwa vitendo vya kihalifu kwa ujumla hapa Zanzibar, vitendo hivyo hivi sasa vinachipua kwa kasi ya ajabu.

Ukisoma, ukitazama na kusikiliza vyombo vya habari kwa nyakati tofauti, kuazia vipindi vya mawio hadi machweo, taarifa zinazotawala ni matukio ya kihalifu ambayo mengine yalikuwa nadra sana kuyasikia yakitokea katika jamii yetu.

Yapo matukio ya kihalifu yaliyotokea katika siku za hivi karibuni ambayo kwa hakika yameifanya jamii ianze kuingiwa na hofu kutokana na watendaji wa vitendo hivyo kupoteza imani.

Kwa mujibu wa kumbukumbu tulizonazo mnamo Septemba 8 mwaka huu kijana mmoja aliyekuwa akitoka kufanya mazoezi huko Tomondo, alicharazwa mapanga na kujeruhiwa pasi na sababu yoyote.

Tukio jengine ni lile la Septemba 11 mwaka huu kijana aliyetambuliwa kwa jina la

Ahmed Juma Makame, mkaazi wa Malindi, alishambuliwa na watu wasioulikana, kumkata miguu na baadae kumtupa eneo la Kisakasaka.

Uhalifu mwengine ni ule uliotokea Septemba 13 mwaka huu ambapo, Yakoub Farouk Yakoub mkaazi wa Mwanakwerekwe, alishambuliwa na watu wasiojulikana na kuvunjwa miguu.

Aidha Septemba 13 mwaka huu, mwanamama mmoja alipigwa mapanga vibaya katika maeneo ya Kikwajuni akiwa njiani kwenda kununua chipsi mnamo majira ya 3 na robo usiku huku wahalifu hao wakiondoka na simu na pesa zake.

Yapo matukio mengine ya kihalifu yaliyotokea miezi ya Juni, Julai na Agosti mwaka huu yakiwemo ya madereva bodaboda kugeukiwa na mateja wao na kupokonywa vyombo hivyo wakitishiwa kwa silaha za jadi.

Katika matukio hayo lipo tukio lililotokeza mwezi Septemba mwaka huu ambapo familia moja nyumba yao iliunguzwa moto usiku ulioathiri chumba kilicholala watoto wawili ambao waliojeruhiwa na zipo taarifa kwa mmoja kati ya watoto hao wamefariki.

Matukio ya uhalifu mkubwa katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita mengi yametokea katika Mkoa wa Mjini Magharibi na kwa kiasi kikubwa yanaaza kuiaminisaha jamii kuwa vile vikundi vya kihalifu vinachipua tena.

Hatusemi kwamba mikoa mingine hakuna halifu hapana, upo kama ilivyoripotiwa baadhi ya matukio huko mkoa wa Kusini Unguja baadhi ya vijana wa kiume kuwashambuliwa wapenzi.

Mara nyingi ukatili unaofanywa na watu waliomo kwenye mahusiano huwa tunaambiwa kuwa unatokana na ‘wivu wa mapenzi’ msamiati ambao kamwe sisi hatukubaliani nalo.

Wivu wa mapenzi ambao tunamzuri wa Kama wivu wa mapenzi kwanini mshambuliaji alighadhibika ajiui yeye mwenyewe?

Hapo pia hatujaingiza mtukio ya udhalilishaji wa kijinsia ambapo kwa mujibu wa ripoti nyingi kama sio zote kutoka Jeshi la Polisi na Ofisi ya Mtakwimu mkuu wa serikali wilaya zinaoongoza matukio hayo ni Magharibi ‘A’ na Magharibu ‘B’.

Hatusemi haya kwa kalaumiani, hasa ikizingatiwa kuwa jukumu la msingi la kuondosha uhalifu katika jamii ni la kila mwana jamii sio la kamati za ulinzi, usalama na jeshi la polisi pekee.

Hata hivyo, mamlaka zilizopewa nguvu za kisheria katika kudhibiti vitendo vya kihalifu na uvunjifu wa amani, viongeze nguvu na bila shaka jamii iko tayari kushirikiana ili kuvimaliza vitendo hivyo.