TOKYO, JAPANI
MASHIRIKA manne yasiyokuwa ya kiserikali nchini Japani yametoa wito kwa serikali ya nchi hiyo kuwasaidia raia wa Afghanistan waliosaidia katika shughuli za msaada na sasa wangependa kuhama.
Serikali inafanya kazi kuwahamisha watu wapatao 500 ambao bado wamekwama nchini Afghanistan, wakiwemo raia wa nchi hiyo wanaofanya kazi kwenye ubalozi wa Japani.
Maofisa kutoka shirika la Pathways Japan na mashirika mengine matatu yasiyo ya kiserikali walifanya mkutano na wanahabari kwa njia ya mtandao.
Walisema juhudi za serikali za uhamishaji hadi kufikia sasa zimeangazia mno watu walio na uhusiano na ubalozi au serikali.
Mashirika hayo yaliiomba serikali kutoa usaidizi kwa raia wa Afghanistan waliosaidia taasisi binafsi na walio na uhusiano fulani na Japani, wakiwemo waliosomea nchini Japani na wanafamilia wao.