TOKYO, JAPANI

NHK imebaini kuwa serikali ya Japani inapanga kufanya majaribio wakati ikielekea kuregeza masharti ya kukabiliana na virusi vya korona.

Kuregezwa kwa masharti hayo kutahusisha watu wenye hatari ndogo ya kueneza virusi, wakiwemo waliochanjwa au kutokutwa na virusi.

Kupitia majaribio hayo,serikali inataka kubaini changamoto zinazoweza kuibuka katika kuregeza vizuizi hivyo.

Serikali inapanga kufanya majaribio hayo kwenye migahawa, baa, maeneo madogo kunakofanyika matamasha, nyumba ndogo za maonesho na matukio makubwa.

Katika majaribio hayo,rikodi za watu waliochanjwa zitakaguliwa,orodha za wageni zitaandaliwa na viwango vya uingizaji hewa safi vitapimwa.

Majaribio hayo yatafanyika huku vizuizi vya idadi ya watu na saa za kufanya kazi vikiwa vimeregezwa.

Serikali itatafuta ushirikiano wa kufuatilia tafiti ili kubaini ikiwa watu waliambukizwa.Serikali inapanga kutoa taarifa zaidi hivi karibuni.