NA JOSEPH DAVID, SCCM
TIMU ya JKT Tanzania inayoshiriki ligi daraja la kwanza msimu ujao inatarajia kuanza mazoezi rasmi mapema wiki ijayo kwenye uwanja wa Isamuyo jijini Dar es salaam.
Kocha mkuu wa timu hiyo Mohamed Abdallah Bares alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na gazeti hili kisiwani Unguja ambapo yupo kwa mapumziko.
Bares alisema tayari amekamilisha zoezi la usajili kwa kuongeza maeneo muhimu yaliyoonekana kuwapa changamoto msimu uliopita, ikiwemo eneo la kipa, beki wa kushoto na washambuliaji.
Aidha, Bares alisema wamejidhatiti kurejea tena ligi kuu Tanzania bara kwa kishindo, huku wakisahihisha walipokosea msimu uliopita mpaka ikawapelekea kushuka daraja.
Alito wito kwa makampuni na mashirika mbalimbali kudhamini na kufadhili mpira wa Zanzibar, kwani kuna vijana lukuki wenye vipaji na uwezo mkubwa ambao wanahitaji kusaidiwa.
Timu ya JKT Tanzania ni miongoni mwa timu nne zilizoshuka daraja msimu uliomalizika, nyingine ni Ihefu FC, Gwambina FC na Mwadui FC.