ZASPOTI
BONDIA, Oleksandr Usyk ndiye bingwa mpya wa WBA, WBO, IBF na IBO baada ya kumchapa, Anthony Joshua kwa pointi kwenye pambano kali lililopigwa usiku wa kuamkia jana.
Pambano hilo lilipigwa kwenye uwanja wa Tottenham Hotspurs jijini London.
Usyk raia wa Ukraine alishinda kwa pointi 117-112, 116-112, na 115-113, hivyo kuondoa uwezekano wa Joshua kupambana na Tyson Fury kwa ajili ya pambano la kuunganisha mikanda yote mikubwa ya uzito wa juu.
Joshua anatarajiwa kutumia kipengele cha pambano la marudiano kati yake na Usyk ili kujaribu kuirudisha mikanda yake aliyoipoteza mbele ya bondia huyo.(AFP).