LONDON, England
BONDIA,Anthony Joshua, amesaini mkataba mpya wa utangazaji wa muda mrefu na Eddie Hearn, ambao utamfanya awe na mtangazaji huyo hadi atakapostaafu mchezo wa ngumi.

Bingwa huyo wa uzani mzito alikuwa mtaalamu wa ngumi akiwa na Hearn mnamo 2013 na atabakia akishirikiana naye na kampuni yake kwa kipindi chote cha kazi yake.

Katika pambano lake dhidi ya Oleksandr Usyk lilifanyika juzi, alionyesha uhusiano uliojengwa kati ya Joshua na Hearn katika mkataba wao mpya.

“Tumejenga misingi mizuri kwa miaka mingi na ninashukuru Matchroom, kampuni, timu, biashara ya familia”.”Hiyo ni aina ya kile kilichonivutia kwenu pia, uadilifu ambao Hearns anao linapokuja jambo la mchezo wa ngumi na biashara”.
“Kwa hivyo, kuwa na Matchroom Sport imekuwa baraka kwangu, familia yangu na timu yangu”, aliongeza, Joshua.(Goal).