NA VICTORIA GODFREY

UONGOZI wa Chama cha Judo Tanzania (JATA) umesema  klabu  za Tanzania Bara, zinaendelea kujipanga vyema kuhakikisha zinafanya vizuri katika mashindano ya Tanzania ‘Weight Categories’ yaliyopangwa kufanyika Septemba 12 mwaka huu visiwani Zanzibar.

Akizungumza na Zanzibarleo Katibu Mkuu wa JATA Innocent Malya,alisema klabu zinaendelea  kujiandaa na mazoezi ya kujiweka sawa  tayari kwa mapambano.

Alisema lengo ni kuhakikisha wanakwenda kufanya vizuri na kuchukua kombe na ubingwa kwa ujumla .

“Maandalizi ya klabu zetu za Bara zinaendelea na mazoezi ,lakini kwa sasa hatujapata takwimu sahihi za zipo zitashiriki ,hivyo tutajua hivi karibuni,” alisema  Malya.

Katibu huyo alisema  mashindano hayo hufanyika kila mwaka kwa awamu kwa kushirikisha klabu za Tanzania Bara na Zanzibar.