NA NASRA MANZI, DAR ES SALAAM
KIKAO cha Kamati Ndogo ya Mashindano ya Taifa cup kimeanza jana kwa kuwakutanisha wajumbe mbali mbali, kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kilichofanyika kwenye ukumbi wa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es -Salam.
Kamati hizo ni pamoja na Kamati ya Fedha Mipango na Masoko, Kamati ya Ufundi, Kamati ya Habari na Matukio, pamoja na Kamati kuu Taifa Cup.
Akizungumza mara baada ya kikao hicho Mkurugenzi Idara ya Michezo Tanzania Alex Mkenyenge alisema lengo la kikao ni kupanga na kuangalia maeneo ambayo yatawakilishwa katika kamati kuu ya mashindano, lakini pia kwa ajili ya kujitayarisha na maandalizi na hatimae tukio zima la mashindano ya Taifa cup kukamilika vizuri.
Kwa upande wake Mratibu wa mashindano hayo Henry Lihaya aliwataja wajumbe wa kamati hizo ambapo kamati ya Fedha Mipango na Masoko Willium Kallaghe NBC, Eunice Chiume,Maliale, Gabriel Ndelumaki, Jumanne Njovu, Peter Simon,Mbaki Mutahaba, Raina Matowo,Oscer Zablon, Fadhil Rajab Mrisho,Nawwal Abdulla, Kamati ya Ufundi Jackson Taweka, Wilfred Kidau, Michael Mwita,Ali Ussi Bakari, Michael Warsha,Sabri Mohamed, Muhidin Yassin.