NAIROBI, KENYA

SERIKALI imeweka sheria mpya inayoelezea msururu wa faini kubwa kwa utelekezaji na unyanyasaji wa watoto, haswa katika mitandao ya kijamii.

Muswada wa Sheria ya Watoto 2021, unataka kufuta Sheria ya Watoto 2001, ili kutoa adhabu ya kumnyima mtoto haki ya kuishi, ustawi na maendeleo.

Muswada huo uliodhaminiwa na Kiongozi wa Wengi Amos Kimunya kuchukua hatua dhidi ya ukiukwaji wowote wa haki za watoto na kupuuzwa kwa uwajibikaji wa wazazi.

Baba wala mama wa mtoto hawatokuwa na haki ya juu au kudai dhidi ya mwengine wakati wa kutekeleza jukumu kama hilo la uzazi.

Endapo wazazi wawili wa mtoto wataoa au kuolewa na watu wengine, mzazi anayedhani kuwa ana haki ya kisheria ya mtoto atakuwa na haki ya kutekeleza jukumu la mzazi kwa mtoto.

Muswada huo unaeleza kwamba wangefanya hivyo ama peke yao au kwa pamoja na wenzi wa ndoa.”Watu wawili au zaidi wanaweza kuwa na jukumu la wakati mmoja la wazazi kwa mtoto mmoja.”