NAJAF, IRAQ

AYATOLLAH Sayyid Mohammed Saeed al-Hakeem, mmoja wa viongozi wakuu wa Shia wa Iraq, amefariki akiwa na umri wa miaka 85 katika mji mtakatifu wa kusini wa Najaf.

Ofisi ya Al-Hakeem ilitangaza hapo juzi jioni kwamba alifariki kutokana na matatizo ya kiafya ambayo haikufafanuliwa zaidi.

Familia ya Mohsen al-Hakeem, ililiambia shirika la habari la Associated Press kwamba al-Hakeem alifariki katika hospitali ya Al Hayat huko Najaf alikopelekwa baada ya kupata mshtuko wa ghafla wa moyo.

Taarifa zilisema kuwa mazishi yalifanyika jana Jumamosi huko Najaf eneo lililo karibu na mji mtakatifu wa Karbala.

Kwa mujibu wa chanzo cha ndani ya ofisi yake ilisema shirika la habari la AFP, Rais wa Iraq Barham Salih katika taarifa yake alitoa heshima kwa “mtu mashuhuri” katika Uislamu na jamii ya washia.

Nayo Marekani ilitoa salamu za pole ambapo katika taarifa kutoka kwa ubalozi wake huko Baghdad, ilisema kuwa alichukuliwa kuwa miongoni mwa viongozi wakuu wa dini ya Shia.

Kabla ya kifo chake, alikuwa mmoja wa viongozi wa juu wa Ayatollah wanne wa Hawza, wakuu wa mashia huko Najaf, pamoja na wakfu wa Ayatollah Ali al-Sistani, kiongozi mkuu wa kiroho wa Shia wa Iraq.

Babu yake Mohsen Al-Tabataba’i Al-Hakeem, alikuwa msomi na mmoja wa wanafikra mashuhuri wa Uislamu wa Shia. Baba yake alikuwa Muhammad Ali al-Hakeem, mmoja wa viongozi wa Shia walioheshimiwa sana huko Najaf.Al-Hakeem aliwahi kufungwa jela kati ya 1983 na 1991 chini ya serikali ya Saddam Hussein.