BOGOTA, COLOMBIA

OFISA wa afya nchini Colombia amesema aina mpya ya kirusi cha corona maarufu kama “Mu” kilichogunduliwa nchini humo mwezi Januari, ndiyo kinachosambaa zaidi nchini humo na kinahusika na wimbi baya zaidi la janga la corona.

Ofisa huyo wa afya Marcela Mercado,alisema kirusi cha “Mu” kinahusika na wimbi kali la tatu la maambukizi kati ya April na Juni.

Wakati wa kipindi hiki, ikiwa na takribani vifo 700 kila siku, karibu theluthi mbili ya vipimo vilivyofanywa kutoka kwa watu waliofariki vilionesha waliambukizwa kirusi cha Mu. ]

Shirika la afya duniani WHO, lilikitangaza kirusi cha Mu, chenye jina la Kisayansi B.1.621, kuwa kirusi muhimu.

WHO ilisema kirusi hicho kina mabadiliko yanayoonesha hatari ya kuishinda nguvu ya chanjo na kwamba utafiti zaidi unahitajika kukielewa.