BARCELONA, Hispania
KOCHA wa Barcelona, Ronald Koeman, amesema, waamuzi wa Hipsania wanaweza kutoa kadi nyekundu pasipo sababu baada ya yeye na kiungo wake, Frenkie de Jong, kutolewa nje kwenye mechi dhidi ya Cadiz iliyoishia kwa sare 0-0 juzi.
Barcelona walihitaji kuondoka na ushindi katika dimba la Estadio Nuevo Mirandilla, lakini, kadi nyekundu aliyooneshwa De Jong kunako dakika ya 65 ilizima matumaini yao.
Miamba hiyo ya Catalunya mpaka sasa imetoka sare katika michezo mitatu kati ya mitano ya ‘La Liga’ na wakiwa na pointi saba nyuma ya mahasimu wao wanaongoza, Real Madrid inayoshika nafasi ya kwanza huku Barcelona ikiwa ya saba.
Koeman kwa sasa muelekeo wa kibarua chake haueleweki Nou Camp baada ya kuanza msimu vibaya na alizungumza na waandishi na kunukuliwa.”Sitazungumzia matatizo yangu, inawezekana kubakia kama nitashinda na ikiwa nitaendelea kupoteza klabu haina budi kutafuta kocha mwengine”.
“Nilisalimiana na rais Joan Laporta muda mfupi kabla kuondoka hotelini, nina uhakika tutapata siku zaidi za kuzungumza, ikiwa klabu watataka kuzungumza”.Barcelona inajiandaa na mchezo mwengine na Levante katika dimba la Nou Camp kesho.(Marca).