LONDON, England
MIPANGO ya klabu za Arsenal na Tottenham Hotspurs za jijini London za kumuwania mshambuliaji wa Inter Milan, Laurato Martinez, imegonga mwamba.Klabu hizo ambazo zina upinzani wa jadi, zilitajwa kumuwania mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Argentina mwenye umri wa miaka 24 wakati wa usajili wa majira ya kiangazi mwaka huu 2021.

Laurato, amesitisha mpango wa klabu hizo, baada ya kukubali kuongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia Inter ambapo katika mkataba huo mpya hakuna kipengele cha kuruhusiwa kuondoka.

Kwa sasa usajili wa Martinez utakuwa mgumu kutokana na kukubali kuongeza mkataba mwengine, ambao utamuweka na kufungumana na klabu kwa muda mrefu kukiwa hakuna kipengele kitakachomuwezesha kuondoka.

Martinez alikuwa ana thamani ya pauni milioni 55, wakati akiwa amebakisha miaka miwili katika mkataba wake kwenye dirisha la usajili lililopita.Kwa sasa thamani yake itapanda zaidi kulingana na mkataba, ambao atakwenda kutia kusaini, ingawa bado haijawekwa wazi ni lini, lakini, imesemwa ni siku chache zijazo.