BERLIN, UJERUMANI

VIJANA kote duniani wameanza kuandamana kudai hatua za haraka zichukuliwe kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Hayo ni maandamano ya kwanza makubwa yanayofanywa na vijana hao tangu lilipozuka janga la Covid-19.

Maandamano hayo yanafanyika wiki tano kabla ya mkutano wa kilele wa mazingira wa Umoja wa Mataifa wa COP26.

Waandamanaji wanalenga kushinikiza hatua zaidi za kimazingira zichukuliwe na viongozi wa dunia kupunguza kwa kiasi kikubwa gesi zinazochafua mazingira na kusababisha ongezeko la joto duniani.

Vuguvugu la vijana wanaharakati wa mazingira, la Friday for Future, limesema maandamano hayo yameanza barani Asia na yamepangwa katika maeneo zaidi ya 1,500.

Mamia kwa maelfu ya washiriki wanatarajiwa kujitokeza nchini Ujerumani katika maeneo zaidi ya 400.