NA MWANDSHI WETU

Wakati zaidi ya wanamichezo 1,000 wakiondoka Unguja juzi kwenda pemba kwa ajili ya Tamasha la 57 la Elimu bila Malipo, mabingwa wa soka kanda ya Unguja skuli ya Chuini Sekondari juzi waliagwa rasmi na kupewa maelekezo mahsusi.

Hafla ya kuagwa kwa timu mhiyo na viongozi wake iliyoambatana na makabidhiano ya vifaa vya michezo, ilifanyika katika skuli hiyo na kuongozwa na sheha wa sheha hiyo Mohamed Shehe Kheri.

Akizungumza katika hafla hiyo, sheha huyo aliwataka wachezahi hao mbali ya kudhamiria kurudi na ubingwa, pia wazingatie nidhamu.

Alisema ushindi hautopatikana bila ya kuwa na nidhamu ya mchezo ndani na nje ya iuwanja hivyo wanapaswa kuzingatia maelekezo watakayopatiwa na viongozi wao.

“Muda wote mtakapokuwa huko mjue kuwa mnawakilisha skuli yenu lakini pia shehia yenu na mtakapofanya vyema kwa niaba ya viongozi wenzangu nawaahidi kuwapa zawadi kubwa,” alisema Kheri.

Aidha aliwataka kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa corona ili waendelee kuwa salama na kufanikisha lengo lao katika mashindano hayo.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake, nahodha wa timu hiyo ahmed Suleiman khamis, aliwashukuru viongozi wa shehia hiyo kwa kuwapa moyo.

“Nataka niwaahidini wazazi na vingozi wetu, kama tuliweza kuwa mabingwa wa wilaya, mkoa na kanda ya Unguja, pia tunaweza kuwa mabingwa wa taifa hivyo tunachoomba muendelee kutuombea,” alisema Khamis.

Kikosi cha wachezaji 20 kikiwa na wachezaji na viongozi cha timu hiyo kiliondoka Unguja jana asubuhi kushiriki tamasha hilo ambalo linaloshirikisha michezo na shughuli mbali mbali za kitaaluma.