NA MWAJUMA JUMA

KOCHA msaidizi wa timu ya soka ya Mafunzo Abdalla Bakari ‘Edo’ amesema matokeo ya kufungwa bao 1-0 nyumbani yamewaathiri lakini wanajipanga kwenda kupambana .

Edo aliyasema hayo mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika na timu ya GD Inter Clube uliochezwa mwishoni mwa wiki  uwanja wa Amaan.

Alisema katika mchezo huo wachezaji wake walipambana lakini walikosa bahati ya kufunga.

“Wachezaji walijituma kadri ya uwezo wao tumepoteza nafasi na sio bahati yetu katika mchezo na naamini tukirudi tena tutafanya vizuri”, alisema.Hata hivyo alisema katika mchezo huo wamewaona wapinzani wao wanavyocheza, watatumia udhaifu huo kufunga mabao.

“Wakati tunacheza nao hatukujua wanachezaje lakini sasa hivi tumewaona tutapata somo la kwenda kujifunzia wachezaji wetu tuweze kurekebisha mechi inayofuata mbele”, alisema.