RABAT, MOROCCO
MAHAKAMA ya juu ya Umoja wa Ulaya imeifuta mikataba miwili ya biashara na Morocco, ambayo ilikuwa inairuhusu nchi hiyo kufanya biashara zake kutoka Sahara Magharibi.
Uamuzi huo unaweza kuharibu uhusiano kati ya Umoja wa Ulaya na Morocco.
Mahakama ya Haki ya Ulaya, ECJ ilisema hatua ya kufuta mikataba ya kilimo na uvuvi imechukuliwa baada ya vuguvugu la kisiasa la Polisario linalodai uhuru wa Sahara Magharibi, kufungua kesi kuipinga mikataba hiyo iliyosainiwa mwaka 2019.
Morocco inalidhibiti eneo la Sahara Magharibi, lakini Algeria imekuwa ikiiunga mkono Polisario.
Mahakama hiyo ilibaini kuwa chama cha Polisario kilikuwa kinatambuliwa kimataifa kama mwakilishi wa watu wa Sahara Magharibi na Umoja wa Ulaya haukuhakikisha kuwa umepata idhini ya watu wa Saharawi kabla ya kufikia makubaliano na Morocco.