LONDON, UINGEREZA

SHIRIKA la hali hewa la Umoja wa Mataifa limetahadharisha kuwa majanga ya kimazingira yanaikabili dunia mara nne au tano zaidi na kusababisha uharibifu mara saba zaidi ya ilivyokuwa katika miaka ya 1970.

Shirika hilo linasema kwamba majanga haya yanawauwa watu wachache kwa sasa.

Katika miaka ya 1970 na 1980 majanga haya yalikuwa yanauwa wastani ya watu 170 kila siku kote duniani ila kuanzia mwaka 2010 majanga hayo yamekuwa yakiuwa watu 40 kwa siku duniani.

Ripoti hii ya Umoja wa Mataifa inakuja wakati ambapo dunia imeshuhudia majanga kadhaa huku Marekani ikikumbwa na kimbunga kikali cha Ida na mioto mikali ya msituni iliyochochewa na kipindi cha ukame.

Ripoti hiyo inasema katika miaka ya 1970 dunia ilikumbwa na wastani wa majanga 711 kwa mwaka ila kuanzia mwaka 200 hadi 2009 majanga hayo yaliongezeka na kufikia zaidi ya 3,500 kwa mwaka au majanga kumi kwa siku.