UTAFITI uliofanywa na kampuni ya MSN Money inayohusika na mikataba ya usafirishaji wa pesa, hisa na biashara ya nyumba za makaazi duniani umebainisha kuwa orodha ya majengo yenye gharama kubwa zaidi duniani.

Utafiti huo umefichua kuwa nyumba 30 za gharama ya juu zaidi duniani, huku Saudi Arabia ikiongongoza kwa kuwa na majengo mawili yenye thamani ya juu zaidi yaliyopo katika mji mtakatifu wa Makka.

Masjid Al-Haram

Utafiti huo uliofanyika mwaka 2019, ulibaini kuwa msikiti wa Ka’bah uliopo Makka, na masjid al-Haram, ndio majengo yenye gharama zaidi duniani na makubwa zaidi.

Kupanuliwa kwa msikiti huo kwa miaka kadhaa kumeuongezea thamani zaidi kuliko jengo jingine lolote duniani na kulingana na MSN Money, msikiti huo una thamani ya dola bilioni 100.

Eneo hilo takatifu zaidi katika dini ya kiislamu na msikiti mkubwa zaidi duniani wa Ka’bah mjini Makka nchini Saudi Arabia, ambao una uwezo wa kuwapokea watu zaidi ya milioni nne wakati wa ibada ya hija, limekadiriwa kuwa thamani hiyo.

Jengo la Abraj Al-Bait ambapo pia lipo katika mji wa Makka, ambalo linajumuisha hoteli, makaazi ya kifahari na maduka, ndilo la pili lenye thamani kubwa zaidi duniani likiwa na thamani ya dola bilioni 16.

Jengo la Abraj Al Bait, ambalo lililopo karibu na msikiti wa Ka’aba, kwa mujibu wa zinaeleza kuwa lililojengwa mnamo mwaka 2012, limechukua nafasi ya pili kuwa jengo lenye thamani kubwa zaidi duniani likiwa na thamani hiyo.

Abraj Al Bait lilijengwa kwa garama ya dola bilioni 15 kwa ajili ya kuwahifadhi mahujaji hususan viongozi na matajiri wakiwemo wanaokwenda kutekeleza ibada ya hijja, ambapo zaidi ya hayo ukubwa wake jengo hilo lina saa kubwa zaidi duniani.

Baada ya kufanyiwa tathmini jengo hilo limekamata nafasi ya pili duniani kwa kuwa na thamani kubwa.

Eneo la burudani la Marina Bay Sands liliopo nchini Singapore ni ya tatu kwa kuwa na thamani kubwa duniani, ambapo ripoti MSN Money imeeleza kuwa majengo katika eneo hilo yana thamani ya zaidi ya dola bilioni 6.

Jengo la Marina Bay Sands resort lililopo Singapore lina hoteli na majumba ya kifahari ndilo linalochukua nafasi ya tatu kati ya majengo yenye gharama ya juu zaidi duniani.

Marina Bay Sands, ambalo ujenzi wake ulikamilika mnamo mwaka 2010, lilijengwa kwa garama ya ya dola bilioni 5.5, ambapo thamani yake imepanda katika siku za hivi karibuni.

Makao makuu ya kampuni ya Apple, Cupertino ni jengo la nne lenye thamani kubwa zaidi duniani ambapo ripoti ya MSN Money imebainisha kuwa jengo hilo lina thamani ya dola bilioni 5.

Jengi hilo la kuvutia lipo linalotumiwa kama ofisi na kampuni hiyo ya kutegeneza simu za vifaa vya tenolojia lipo katika katika eneo la Cupertino mjini California nchini Marekani.

Kampuni ya Apple, ambayo ndio kampuni ya gharama zaidi duniani, inasemekana ina mapato ya jumla ya juu zaidi kuliko mali zote zinazomilikiwa na mataifa yanayoendelea.

Si jambo la kushangaza kwamba kampuni ilitumia ilitumia dola bilioni 5 kujenga jengo hilo kubwa la makao yake makuu.

Jengo jengine lenye thamani kubwa zaidi ni Cosmopolitan Building, ambalo lipo katika mji wa Las Vegas, ambapo inakadiriwa jengo hilo lina thamani ya dola bilioni 4.4.

Ikiwa na jumla ya vyumba 3,027 vya kulala wageni jengo la hoteli ya Cosmopolitan lina thamani ya dola bilioni 3.9 na ujenzi wake ulikamilika mnamo mwaka 2009.

Jengo hilo lina kasino kubwa, chumba cha mikutano chenye viti 3,200- ni jingo la tano lenye gharama zaidi duniani.

Jengo la New York-World Trade Center linashikilia nafasi ya sita katika orodha ya majengo yenye ghali zaidi duniani kulingana na kampuni ya MSN Money.

Ujenzi wa One World Trade Center ulikamilika mnamo mwaka 2012 kwa garama ya dola bilioni 3.8 (£ 2.7bn), lakini kwa sasa thamani yake imepanda hadi zaidi ya dola bilioni 4. Jengo hilo kwa sasa ndilo linaloshikilia nafasi ya kwanza kwa ukubwa nchini Marekani.

Jengo la bunge la Bucharest: Dola bilioni 3.9 ambalo lilizinduliwa mwaka 1984, sasa lina thamani ya dola bilioni 3.9, lipo nchini Romania.

Jengo la hoteli-Emirates Palace Hotel Building, lililoko Abu Dhabi ni jengo jengine lenye thamani kubwa ambapo linathamani ya dola bilioni 3.8.

Jengo hilo la hoteli ambalo muundo wake unafanana na ule wa kasri ya ufalme ya Dubai lina jumla ya vyumba vya kulala 397 pamoja na maduka makubwa (malls) na madogo na migahawa ya kifahari.

Thamani ya jengo hilo ambalo ujenzi wake ulikamilika mwaka 2005, likikadiriwa kuwa na thamani dola billioni 3, kwa sasa thamani yake ni zaidi.

Wynn Resort, Las Vegas jengo jilo lina thamani ya dola bilioni 3.4, hiyo ni miongoni mwa moja wapo ya hoteli nzuri zaidi duniani likiwa katika kundi la kasino kubwa katika za Las Vegas.

Mwaka 2005 jengo la Wynn Park lilizinduliwa, thamani ya jengo hili lenye vyumba 2,716-likikadiriwa kuwa ni dola bilioni 2.7, sasa thamani yake ni zaidi ya dola bilioni 3.4.

Kasri la Mfalme wa Brunei Istana Nurul Iman ni jengo jengine lenye thamani kubwa lilikadiriwa kuwa na thamani ya dola bilioni 3.3. Kasri la Brunei lililojengwa 1984 kwa garama ya dola bilioni 1.4 billion, ndio kasri kubwa zaidi duniani ambalo bado limesimama kama kasri.

Jengo la kasri la serikali ya Brunei likiwa na vyumba 1,788 na ukumbi mkubwa wa mikutano unaoweza kuwapokea watu 5,000. Sultan wa Brunei Hassanal Bolkiah ni mmoja wa watu matajiri zaidi duniani.

Hata hivyo, utafiri huo uliofanywa na MSN Money umekadiria kwamba jengo la Burj Khalifa, lililopo mjini Dubai katika nchi ya Falme za Kiarabu (UAE) linachukua nafasi ya 30 katika orodha ya majengo ghali zaidi duniani, licha ya kwamba ndio jingo refu kuliko majengo yote duniani.