NA ZAINAB ATUPAE

MRATIBU wa mashindano ya resi za ngalawa Mohamed Abdalla ‘Toza’,amewataka mahodha kujitokeza kwa wingi  kushiriki mashindano hayo ili kuleta ushindani zaidi.

Toza aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari huko Fumba baada ya kumalizika  kwa mashindano ya resi za ngalawa ziliozofanyika katika bahari ya Fumba wilaya ya Magharibi ‘B’.

Alisema lengo la kuanzisha mashindano hayo ni kutoa elimu kwa wavuvi ambao wanakwenda dago na kuzitekeleza familia zao,jambo ambalo sio sahihi na nikosa kisheria.

Aidha alisema mashindano hayo yalishirikisha ngalawa tisa ambapo zilitakiwa kushiriki ngalawa 15 kwa mujibu wa taarifa ilivyotoka.

Akitangaza matokeo kwa washindi,alisema mshindi wa kwanza ilikuliwa ni ngalawa ya Utaisikia iliokuwa ikiendeshwa na nahodha Shaban Ramahan,huku ngalawa ya Dege ilifanikiwa kuwa mshindi wa pili iliokuwa ikindeshwa na Abdul Said.

Mshindi wa tatu ni galawa ya Dibwedibwe iliokuikiendeshwa na nahodha Abrahman Khamis.Aidha alisema kwa upande wa zawadi mshindi wa kwanza aliondoka na 200,000,mshindi wa pili 150,000 na wa tatu aliondoka na100,000.