TOKYO, JAPANI

WIZARA na idara za Japani zimewasilisha maombi yao ya bajeti ya mwaka ujao wa fedha.Maombi hayo ni jumla ya karibu trilioni 110 au takribani dola trilioni moja ambayo ni rikodi kwa mwaka wa nne mfululizo.Ombi kubwa linatoka Wizara ya Afya, Kazi na Ustawi wa Jamii.

Inaomba karibu dola bilioni 310, zikiwa ni za juu zaidi kuwahi kuwasilishwa na wizara au idara.Matumizi kwenye mipango ya tiba na huduma za uuguzi na mipango mengine ya usalama wa jamii yanaendelea kuongezeka kufuatia ongezeko la wazee.

Gharama ya kulipa deni la umma la Japani pia imeongezeka mno.Fidia na malipo ya riba kwenye dhamana za serikali zimefikia zaidi ya dola bilioni 270.

Hilo ni ongezeko la dola bilioni 50 zaidi kuliko bajeti ya awali ya mwaka wa sasa wa fedha.Wizara ya Ulinzi inaomba takribani dola bilioni 50.

Zinajumuisha gharama ya kununua meli za kusafirisha maafisa wa ulinzi, huku shughuli zinazoongezeka za majini za China zikiangaziwa.