NA MWAJUMA JUMA

TIMU ya soka ya Mapembe City inayoshiriki michuano ya Yamle Yamle imesonga mbele hatua ya 16 bora, kwa ushindi wa penalti 5-4 uliochezwa juzi uwanja wa Amaan.

Timu hizo zilifikia hatua ya kupigiana mikwaju ya penalti baada ya dakika 90 kumalizika bila ya kufungana.

Tayari timu 10 zimeshatangulia hatua hiyo ya 16 bora zikiwemo Mboriborini mabingwa watetezi, Jamaica, Angaza FC, Uzi City, Chilo combine, Mazombi FC, Kisauni City, Guzoni FC na Mapembe City.

Michuano hiyo leo itahamia katika kiwanja cha Ngome ambapo kutakuwa na mchezo kati ya Go Back na Bridge Star.