ZASPOTI
NEYMAR aliangua kicheko baada ya mashabiki wa soka kudai kwamba amekuwa mzito na kukosolewa kuwa hayupo katika umbo zuri la kucheza soka.

Nyota huyo alicheza dakika zote 90 katika mchezo wa wiki iliyopita wakati Brazil ikipata ushindi mwembamba dhidi ya Chile katika kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar.

Vyombo vya habari vya Ufaransa vilisema kwamba hayupo katika umbo zuri baada ya ushindi wa PSG dhidi Reims wiki iliyopita, hali iliyomsukuma kujibu baada ya kucheza akiwa na Brazil.

Neymar aliposti katika ‘Instagram’ habari yake, akisema wakati wa mechi ya Chile: “Tumecheza vizuri? Hapana! Tumeshinda? Ndiyo!”
Kisha akaelezea kukosolewa kwake kwa uzito alionao: “Kipimo cha fulana kilikuwa saizi kubwa, nipo katika uzito wangu, mchezo ujao nitaagiza ‘M’ huku akiwa ameweka katuni za vicheko.(AFP).