NA VICTORIA GODFREY

TAMASHA la Michezo la Wanawake la Tanzanite limezidi kushika kasi kwa timu za michezo mbalimbali kuchuana vikali katika Uwanja wa Makapa Dar es Salaam.

Tamasha hilo ambalo lilianza jana kwa kongamano na  limeshirikisha timu za wanawake za michezo ya kikapu ,wavu,mpira wa mikono ,Riadha,netiboli na michezo ya jadi.

Matokeo ya michezo iliyochezwa ya riadha mita 100 nafasi ya kwanza imechukuliwa na Hynes John,akifuatiwa na Winfrida Makenji na nafasi ya tatu ni Kazija Hassan wote Zanzibar, mita 200 Emmy Hosea, nafasi ya pili Nasra Abdallah na ya tatu Neema Ally wote kutoka Zanzibar.

Matokeo mengine  mita 400 washindi  nafasi ya kwanza Jane Maiga,akifuatiwa na Shuema Ally na nafasi ya tatu Gaudensia Maneno Pwani,wakati mita 800 Aisha Lubuva akishika nafasi ya kwanza,akifuatiwa na Gaudensia Maneno kutoka Pwani na nafasi ya tatu ilikamatwa na Hamida Nasoro kutoka JKT.

Mbio za mita 1500 washindi nafasi ya kwanza ilienda kwa Transfora Mussa wa JKT,huku nafasi ya pili ikishikwa na Cesilia Ginoka na nafasi ya tatu ikimaliziwa na Regina Deogratius  kutoka Pwani.

Katika Mpira wa Kikapu kwa watu wenye Ulemavu  timu ya Tembo iliibuka Bingwa ,huku Dar city ilikamata nafasi ya pili