WASHINGTON, MAREKANI

SHIRIKA la Upelelezi la Marekani, FBI limesema mauaji nchini humo yameongezeka kwa asilimia 29.4 kwa mwaka 2020.

Kwa mujibu wa ripoti ya uhalifu ya FBI, asilimia 77 ya mauaji yalifanywa kwa kutumia silaha za moto, kutoka asilimia 74 za mwaka 2019.

Kwa ujumla uhalifu kama vile mauaji, ubakaji, unyanyasaji dhidi ya wanawake uliongezeka kwa asilimia 5.6 mwaka 2020, na ujambazi na wizi ulipungua kwa asilimia 7.8.

Matukio ya mashambulizi yaliongezeka kwa asilimia 12.

Mji wa Houston kwenye jimbo la Texas, umeshuhudia ongezeko la asilimia 55 la mauaji ya kutumia bunduki, ambapo visa viliongezeka kutoka 221 kwa mwaka 2019 hadi 343 mwaka 2020.

Kulingana na takwimu za Benki ya Dunia, kulikuwa na mauaji ya asilimia 6.5 kwa wakaazi 100,000 wa Marekani mwaka 2018, ikilinganishwa na 35 Mexico, 27 Brazil, wanane Urusi na moja kwa watu 100,000 Ufaransa na Ujerumani.