MIAMI, Marekani
PAMOJA na kustaafu ngumi za kulipwa, bondia Floyd Mayweather Jr, ametajwa mwanamasumbwi bora nambari moja duniani.

Mmarekani huyo ametajwa kwenye orodha ya mabondia wote wa dunia katika kila uzani.
Mayweather Jr ambaye mara ya mwisho alipanda ulingoni Juni mwaka huu ameendelea kuwa namba moja duniani katika orodha ya mabondia wanaondelea kupigana na

waliostaafu akiwa na pointi 3,568 kwenye mapambano 50 aliyocheza na kushinda yote.
Mpinzani wake, Manny Pacquiao anayepigania pia uzani wa ‘welter’, licha ya kutoonekana ulingoni kwa muda mrefu amekamata nafasi ya nne katika orodha hiyo.

Bondia raia wa Mexico, Saul Alvarez, ametajwa kwenye nafasi ya 10 akiwa na pointi 1,159.
Wengine walioingia kwenye orodha ya mabondia bora kwa mujibu wa Boxrec ni Ezzard Charles, aliyekamata nafasi ya pili na Bernard Hopkins amehitimisha tatu bora.
Wengine ni Andre Ward, Joe Calzaghe, Lennox Lewis, Archie Moore, Wladimir Klitschko na Anthony Joshua.(AFP).