BERLIN, UJERUMANI
KANSELA wa Ujerumani, Angela Merkel amempongeza mgombea wa ukansela wa chama cha Social Democratic, SPD Olaf Scholz kwa kushinda uchaguzi uliofanyika Jumapili.
Taarifa iliyotolewa na ofisi ya Merkel ilieleza kuwa kansela huyo anayeondoka madarakani, aliwasiliana binafsi na Scholz waziri wake wa fedha.
Ofisi hiyo pia ilisema Merkel na mawaziri wataendelea na majukumu yao hadi serikali mpya ya shirikisho itakapoundwa na kuchukua rasmi madaraka.
Kansela Merkel ataendelea kutekeleza majukumu yake ikiwemo kufanya ziara za nje na kuhudhuria mikutano ya viongozi wa serikali wa nchi nyengine.
Aidha, shirika la habari la Ufaransa, AFP limeripoti kuwa kiongozi wa CDU, Armin Laschet pia amempongeza Scholz.