PARIS, Ufaransa
KLABU ya Paris Saint Germain imethibitisha kwamba Lionel Messi, amepata maumivu na atakosekana kwenye michezo kadhaa ya mabingwa hao wa Ufaransa.

Messi alikosa mchezo wa PSG dhidi ya Metz kwenye dimba la Saint Symphorien na alitolewa katika dakika 75 kwenye mchezo dhidi ya Lyon ambapo miamba hiyo ilishinda 2-1 na kuendeleza mwanzo mzuri.

PSG imeshinda mechi sita kwenye ‘Ligue 1’ ikiongoza kwa pointi 18 dhidi ya Marseille yenye pointi 13 kwenye nafasi ya pili.Nyota huyo ambaye aliacha sintofahamu na meneja wake baada ya kutolewa kwenye dakika ya 75, alifanyiwa vipimo na kukutwa na matatizo ya mfupa wa mguu wake wa kushoto.

Meneja wa PSG, Mauricio Pochettino, alisema, alichukua uamuzi wa kumtoa Messi pale tu, alipohisi ameumia baada ya kuona akijishika zaidi ya mara moja kifundo chake.”
Messi mpaka sasa bado hajafunga goli kwenye ‘Ligue 1’. (AFP).