BLOEMFONTEIN,AFRIKA KUSINI
MKUTANO wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa umetoa ahadi ya kuongeza maradufu jitihada ya kukabiliana na vitendo vya ubaguzi wa rangi duniani kwa zingatio la maazimio ya kongamano ya kupinga ubaguzi wa rangi la 2001 la Afrika Kusini.
Kwa kuufanyia marejeo mkutano huo wa Durban, kulipitishwa azimio ambalo lilionesha kiwango fulani cha kupigwa hatua katika vita dhidi ya ubaguzi wa rangi, ingawa bado kunatajwa ongezeko la vitendo hivyo na kutokuwepo kwa hali ya kuvumiliana kunakowakabili watu wenye asili ya Afrika na makundi mengine.
Katika mkutano maalumu uliofanyika kwa njia ya video, Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa alisema mamilioni ya wazawa wa Afrika ambao waliuzwa utumwani wamebakia katika mkwamo, wanaishi pasipo maendeleo, kukosa fursa, kubaguliwa na umasikini.
Kwa hivyo katika maazimio yake Baraza Kuu ya Umoja wa Mataifa kumezingatiwa masuala ya fidia na haki wenye kubaguliwa, zingatio likiwa athari za utumwa, ukoloni na mauaji ya halaiki, na kuwataka watu wenye asili ya Afrika kutafuta stahiki zao kwa kutumia taasisi za kimataifa.