PARIS, UFARANSA

RAIS wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema kuwa mkuu wa kundi la Dola la Kiislamu tawi la eneo la Sahara huko Afrika Magharibi ISGS, Adnan Abu Walid-Sahrawi ameuwawa na wanajeshi wa Ufaransa.
Katika ujumbe aliouandika kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, Macron alisema, kuuwawa kwa mkuu huyo wa kundi hilo la kigaidi ni mafanikio mengine makubwa katika mapambano dhidi ya makundi ya kigaidi katika eneo la Sahel.
Kundi hilo linalaumiwa kwa mashambulizi mengi ya kigaidi yanayofanywa nchini Mali, Niger na Burkina Faso.Kundi hilo liliwalenga wanajeshi wa Marekani katika mashambulizi ya mwaka 2017.
Agosti mwaka 2017 nchini Niger, mkuu wa kundi hilo la kigaidi aliagiza kuuwawa kwa wafanyakazi sita wa mashirika ya kutoa misaada kutoka Ufaransa, pamoja na madereva wao na waliokuwa wasaidizi wao raia wa Niger.