MOGADISHU, SOMALIA

MKUU wa wilaya ya Bulaburte ya Somalia Ahmed Mahad Nur amesema watu zaidi ya watano wamejeruhiwa katika mripuko wa mabomu yaliyotegwa ardhini uliotokea katika uwanja wa ndege ulioko kwenye mkoa wa Hira katikati ya nchi hiyo.

Nur alisema wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab waliingia kisiri katika uwanja huo uliojengwa upya na kutega mabomu ardhini yaliyoripuka baadaye.

Pia alisema, sehemu ya uwanja huo unaopangwa kuzinduliwa baadaye kufuatia kukamilika kwa kazi imeharibiwa kwa mabomu hayo.