KIEV,UKRAINE

MSAIDIZI mkuu wa Rais wa Ukraine Volodymry Zelensky amenusurika jaribio la mauaji baada ya gari lake kushambuliwa kwa risasi.

Mshauri wa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ukraine, Anton Gerashchenko alisema shambulizi hilo limetokea karibu na kijiji cha Lesniki.

Alisema gari la msaidizi mkuu wa kiongozi huyo, Sergei Shefir lilishambuliwa na zaidi ya risasi kumi na dereva amejeruhiwa vibaya.Anton alisema polisi imeanzisha operesheni maalum kuzunguka Kiev.