PARIS, Ufaransa
LIONEL Messi, alijiunga na klabu ya Paris Saint-Germain wakati wa dirisha la usajili la majira ya joto kama mchezaji huru, lakini, mshahara wa nyota huyo wa kimataifa wa Argentina haukuwekwa wazi na sasa matajiri hao wa Ufaransa wameweka wazi mshahara wa mshambuliaji huyo kwa miaka mitatu ijayo.

Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali zinadai kwamba Messi atalipwa euro milioni 30 kwa misimu miwili ijayo na kiasi hicho kinaweza kufika mpaka euro milioni 40 kama akiongeza mwaka mmoja huko Paris.

Kiasi hicho hakihusiani na mapato binafsi ambayo mchezaji anaweza kupata na bonasi za timu wakati wa kampeni.
Chengine ni kwamba Messi atakuwa akitengeneza kiasi cha euro milioni moja kupitia tokeni ya mashabiki ya PSG ya fedha ya matandaoni.
PSG ilisaini dili na Crypto.com na itapata faida kati euro milioni 25 mpaka 30 kwa mwaka.(Goal).