NA ZAINAB ATUPAE
MWENYEKITI wa klabu ya Shangani, Abrahiman Hussein Salim, amewataka viongozi wenzake kushikamana ili kuiendeleza timu hiyo na kufikia malengo.
Aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na mwandishi wa gazeti hili baada ya kufanya uchaguzi mkuu wa viongozi.

Alisema wakati umefika wa kuibadilisha timu hiyo na kurudisha ilikotokea na kinachotakiwa ni ushirikianona na utendaji kazi nzuri kwa viongozi wenzake.
Alisema, baada ya kuchaguliwa na kuwa mwenyekiti anatarajia kufanya kikao cha pamoja na wachezaji ili kujadili mambo mbali mbali ya maendeleo ya timu hiyo.

Alisema, mkakati yao ni kuiandaa timu hiyo ili miaka miwili iliyokuja kuwarejesha mashabaki wao wote.
Shangani inayoshiriki ligi daraja la pili wilaya ya Mjini Magharibi ambapo msimu uliomalizika iliponea chupu chupu kushuka daraja.