DIRISHA la usajili kwa wanasoka nchini Uingereza mwaka huu lilishia kumuona Cristiano Ronaldo akirejea katika klabu yake zamani ya Manchester United katika hali ambayo haikutarajiwa wengi.
Pamoja na Manchester United kwa muda mrefu kuwa na nia ya kumrejesha tena Old Trafford mchezaji huyo, lakini haikuwezekana, hata hivyo msimu huu amerejea huku wengi wakishangaa.
Kabla ya Manchester United kuthibitisha kumsajili kwa mara nyengine, mchezaji huyo aliyetwaa tuzo tano za Ballon D’Or, taarifa nyingi kwenye mitandao zilieleza kuwa mchezaji huyo alikuwa mbinoni kuelekea Manchester City.
Manchester United walilazimika kuingia kati kumsajili Ronaldo kutoka Juventus ya nchini Italia, baada ya kuwepo fununu kuwa mahasimu wao ambao maskani zao zinatengana umbali wa kilomita nne, Manchester City kutaka kumsajili Ronaldo.
Hadi usiku wa Agosti 26 maofisa wa Old Trafford walikuwa na uhakika kuwa mwanasoka huyo bora mara tano wa dunia anarejea ligi kuu ya Uingereza na anaacha kwenda Etihad na kuelekea Old Trafford.
Hadi usiku wa siku hiyo taarifa zinaeleza kuwa Manchester City walikuwa ama wanafikiria mpango huo wa Ronaldo ama kama inavyoelezwa walikuwa wamemalizana nae, ambapo vyanzo vyingi vinasema walikuwa na nia lakini bado hakukuwa na makubaliano yaliyokamilika.
Kabla ya kuthibitishwa usajili wake, United iliendelea kufuatilia hali ya mambo katika klabu ya Juventus ambayo imepitia wakati mgumu wa kifedha, ambapo baada ya meneja wa Juventus Massimiliano Allegri kuthibitisha kuwa Ronalado anaondoa hapo ndipo United ilipoingilia kati.
Suali liliopo ni kina nani hasa wamefanikisha hadi kuhakikisha Cristiano Ronaldo anarejea Old Trafford badala ya kwenda dimba la Etihad chini ya fundi wa soka Pep Guadiola?
Taarifa za ndani kutoka Old Trafford zinaeleza kuwa meneja wa zamani wa Manchester United mzee Alex Ferguson alihusika kwa kiasi kikubwa kumrejesha tena Manchester Unired mchezaji huo.
Ferguson anaelezwa kuwa ana ukaribu mno na Ronaldo ni mkubwa na kwamba pamoja na kwamba ameondoka klabu hiyo tangu mwaka 2009, bado Ronaldo anamchukuliwa Ferguson zaidi ya bosi wake bali ni mmoja wa watu muhimu kwake.
Kabla ya mwaka huu Ferguson kufanikiwa kumrejesha tena katika klabu hiyo, aliwahi kumtaka alirudi Old Trafford, akijua kwamba atakuwa shujaa wa klabu hiyo na kwamba hali ingempa sifa maalum katika klabu hiyo.
Ukiachilia mbali Sir. Alex Ferguson, watu wengine walioshawishi Ronaldo kurejea Old Trafford ni pamoja na wachezaji wenziwe wa zamani wakiwemo aliyekuwa mlinzi wa kati wa klabu hiyo ambaye kwa sasa ni mchabuzi wa soka Rio Ferdinand.
Wengine waliokoleza kuni hadi Ronaldo kurejea katika klabu yake hiyo ya zamani ni pamoja na nahodha wa zamani wa klabu hiyo na beki wa kushoto Patrice Evra, Darren Fletcher ambaye hivi sasa ni mkurugenzi wa ufundi wa United pamoja na kiungo wa klabu hiyo kutoka nchini Ureno, Bruno Fernandes.
Hata hivyo, inadaiwa yalikuwepo mawasiliano ya karibu baina ya United na wakala wa muda mrefu wa mchezaji huyo, Jorge Mendes.
Tetesi zilipoaza kwamba Ronaldo anataka kujiunga na Paris St-Germain kama alivyosema Solskjaer, United ilikuwa nyuma ya pazia, walihisi kwamba Ronaldo angetamani kubaki Turin kumalizia mwaka mmoja uliosalia kwenye mkataba wake.
Lakini United ilifutuka baada ya kusikia Manchester City wanahusishwa na Mipango ya kumsajili Ronaldo, hapo ndipo masikio yao yaliposimama na kuingilia kati.
Ole Gunnar Solskjaer alisema kwamba Ronaldo anajua kwamba klabu hiyo inamuhitaji kwa muda mrefu. “Sikufikiria Cristiano Ronaldo ataondoka Juventus’‘, Solskjaer alisema. Kumekuwa na uvumi mapema leo na uvumu siku chache zilizopita.
Solskjaer alithibitisha kuwa Bruno Fernandes alikuwa akizungumza na nahodha wake huyo wa timu ya taifa ya Ureno kumuelezea nafasi yake endapo angependa kurejea katika klabu hiyo kwa mara nyengine tena.
Kwa nini Juventus iliamua kumpiga bei Ronaldo? Kocha wa Juventus Massimiliano Allegri haamini kama anaweza kumuita Ronaldo mashine ya ushindi hasa kutokana na umri wake uliofikia miaka 36.
Miamba hao wa Italia hawajafika hata robo fainali ya ligi ya mabingwa tangu Ronaldo awasili Turin na klabu hiyo ya Serie ‘A’ ambayo imeshindwa katika hatua ya 16 bora katika kampeni mbili zilizopita.
Msimu uliopita, walipoteza taji la ligi baada ya kushinda kwa miaka tisa mfululizo na kuingia tu kwenye nafasi za ligi ya mabingwa katika michezo michache iliyopita.
Ronaldo alipigwa ubao na Massimiliano Allegri wakati Juventus ilipotoka sare kwenye mchezo wa serie ‘A’ katika mechi yao ya ufunguzi dhidi ya Udinese, kitu ambacho klabu ilisisitiza ni uamuzi wa pamoja na mchezaji huyo.
Aidha taarifa zinaeleza kuwa Juventus wameamua kumpiga bei Ronaldo kutokana na klabu hiyo kukabiliwa na ukata wa kifedha na kwamba malipo ya mshahara wa Ronaldo yangechangia kukausha akaunti za klabu hiyo.
“Mambo hubadilika, ni sheria za maisha. Juventus inasalia ambacho ndio kitu muhimu. Tunamshukuru kwa kile ambacho amekifanya, pia kama mfano miongoni mwa vijana. Lakini kama nilivyosema, lazime maisha yaendelee”.
Kwanini Ronaldo hakupenda kujiunga na Manchester City wapinzani wakubwa Manchester United timu za mji mmoja ambazo maskani zao zitengana umbali wa kilomita nne tu?
Moja ya jambo ambalo linaeleza kuwa limemfanya Ronaldo kutojiunga na Manchester City ni kutoendana na falsafa za kocha wa timu hiyo, Pep Guardiola. Unaposema kuwa Ronaldo anaendana na falsafa za Guardiola jawabu kubwa ni hapana zadi kuliko kusema ndio.
Lakini unajua atafunga mabao mengi kwasababu watamtengenezea nafasi nyingi, hata kama hatafanya kila kitu atakachoagizwa na Pep. “Tunajua Pep ataondoka mwishoni mwa mkataba wake katika muda wa miaka miwili kwa hivyo ni chaguo la muda mfupi hata hivyo.
Labda ukifuata njia hiyo basi pia utafanya ifanye kazi kwa Cristiano kwa muda mfupi na labda ni Pep ambaye pia atabadilika kidogo kuwa na Cristiano katika timu yake, mradi Cristiano ageuze mchezo wake mwenyewe kwendana na kile Pep anataka”.
Ronaldo alisajiliwa na Manchester United kutoka Sporting Lisbon kwa dau la pauni milioni 12.2 mwaka 2003 na kufanikiwa kufunga magoli 118 katika mechi 292 akiichezea klabu hiyo.