LONDON, England
MABOSI wa Manchester United wameamua kuingia kwenye vita dhidi ya Liverpool na PSG ili kuipata saini ya kiungo wa Ivory Coast na AC Milan, Franck Kessie.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24, amewekewa mipango ya kuhamishwa nchini Italia, mwishoni mwa msimu huu 2021/22, na huenda akawa mbadala wa Paul Pogba ambaye mkataba wake utafikia kikomo mwakani huko Old Trafford.

United imekuwa kwenye sintofahamu ya muda kwa sababu hadi sasa Pogba amegoma kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia Trafford, licha ya kuwekewa ofa mezani.

Kessie ni miongoni mwa wachezaji walioonyesha kiwango bora tangu aliposajiliwa AC Milan mwaka 2019, na msimu huu 2021/22 amecheza michezo mitatu ya michuano yote.
Mkataba wa Kessie na AC Milan unatarajiwa kufikia kikomo mwaka 2022. (AFP).