BERLIN, UJERUMANI
POLISI ya Ujerumani imewakamata watu kadhaa kuhusiana na kitisho cha shambulizi dhidi ya sinagogi la Wayahudi mnamo sikuu ya Yom Kippur.
Watu hao walikamatwa katika operesheni kubwa iliyofanywa na polisi katika mji wa Hagen ulioko mashariki mwa Ujerumani, ambao ulilazimika kuahirisha maadhimisho ya siku hiyo muhimu ya dini ya Kiyahudi kwa hofu ya kitisho hicho.
Awali, polisi walikuwa wamezungumzia kuwepo kwa viashiria vya hatari kuelekea taasisi ya Kiyahudi, lakini baadaye waliondoa tahadhari yao.
Magazeti maarufu ya Ujerumani ya Spiegel na Bild yaliripoti kuwa shirika moja la kijasusi la nchi ya kigeni lilikuwa limeonya juu ya uwezekano wa kijana mwenye umri wa miaka 16 kutoka Syria, kufanya shambulizi la viripuzi kwenye sinagogi hilo.
Magazeti hayo hayakuvinukuu vyanzo vyovyote vya taarifa hizo.Uhalifu unaohusiana na chuki dhidi ya Wayahudi umekuwa ukiongezeka nchini Ujerumani tangu mwaka 2019.