TUNIS, TUNISIA

RAIS wa Tunisia Kais Saied amesema atamteua waziri mkuu mpya lakini hali ya dharura ambayo aliitangaza Julai itaendelea kuwepo.

Alisema hatua hiyo inafanyika kwa msingi wa uongozi wa mpito shabaha ni kujibu matakwa ya raia.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara,Saied alilituhumu bunge alilozuwia kufanya kazi zake kuwa kama soko ambapo wapiga kura wananunuliwa na kuuzwa.

Julai 25, Rais Saied aliivunja serikali, kusimamisha utendaji wa bunge na kuziondosha kinga za wabunge na yeye kujikusanyia madaraka yote, jambo ambalo lilipigiwa kelele na jumuiya ya kimataifa.