LONDON, ENGALND

CRISTIANO Ronaldo nyota wa Manchester United amesema  ameshangazwa na mapokezi ya mashabiki wa timu hiyo huku akifurahia kuanza kazi kwa kutupia mabao katika mchezo wake wa kwanza ndani ya ligi kuu England kwa msimu wa 2021/22.

Ronaldo aliweza kuonyesha makeke yake katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Old Trafford dhidi ya Newcastle United alitupia mabao mawili dakika ya 45 likasawazishwa na Javier Manquillo dakika 56 na lile la pili alipachika dakika ya 62.

Bruno Fernandes alipachika  bao moja dakika ya 80 na Jesse Lingard alipachika bao moja dakika ya 90 huku Ronaldo akisema kuwa haamini alichokiona kwa namna mashabiki walivyokuwa wakiimba jina lake katika mchezo huo uliovuta hisia za mashabiki wengi.

Kocha mkuu wa Manchester United,  Ole Gunnar Solskjaer alisema kiwango ambacho Ronaldo amekionyesha huku akisema ni kuhusu Manchester United na kila mmoja atapata kile anachotarajia.

Kwa upande wa kocha mkuu wa Newcastle United Steve Bruce alisema  wamekasirishwa na matokeo hayo ila ni sehemu ya mchezo.